Kiburi Cha Yanga Kuelekea Mchezo Wa Leo Dhidi Ya Wolayta Dicha Na Utabiri Wa Kikosi Kitakachoanza Leo.


Kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika kati ya Wolayta Dicha dhidi ya Yanga unaotarajiwa kupigwa leo majira ya saa 10 jioni, Klabu ya Yanga kutoka Tanzania ndio klabu yenye nafasi ya kusonga mbele mpaka sasa licha ya kuwa mpira una matokeo yoyote kutokana na ushindi wa awali wa goli 2-0 ilioupata kwenye uwanjwma wa nyumbani

Yanga wapo ugenini kuwakabili Wolayta Dicha  nchini Ethiopia katika mchezo utakaopigwa mjini Awassa na wanatarajiwa kushuka dimbani bila ya kuwa na aliyekuwa kocha wake mkuu George Lwandamina ambaye alikiongoza kikosi katika mchezo wa awali ambao kilipata ushindi. Na badala yake kikosi kwa sasa kitaongozwa na Noel Mwandila kama kocha mkuu huku akisaidiana na Shedrack Nsajigwa  kama kocha msaidizi.

Yanga wana hitaji sare yoyote au ushindi huku wakijihitajika kupata bao la mapa ili kuhakikisha wanajiwelea nafasi nzuri ya kutinga hatu ya makundi kwa mara ya pili.

Hata hivyo Yanga inajivunia mtaji wa wachezaji waliukosa mchezo wa awali ambao ni Obrey Chirwa, Kelvin Yondani, Juma Said na Papy Tshishimbi ambao wamerejea na kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho katika mchezo wa marudiano.

Yanga pia itwakosa wachezaji wake kadhaa ambao ni Ibrahimu Ajibu, Donald Ngoma Na Amis Tambwe hii ni kutokana na sababu tofauti ikiwemo majeraha.

Kikosi Cha Yanga Kinatarajiwa Kuwa Hivi.


  1. Youthe Rostand
  2. Hassan Kessy
  3. Hajji Mwinyi
  4. Abdallah Shaibu “Ninja”
  5. Kelvin Yondani
  6. Juma Said
  7. Papy Tshishimbi
  8. Yusuph Mhilu 
  9. Pius Buswita 
  10. Obrey Chirwa
  11. Emmanuel Martin

Ikumbukwe kuwa mchezo huo utaonyeshwa mubashara kupitia Azam TV.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.