Simba Kuanza Kuziwinda Pointi Tatu Za Lipuli Fc Leo.



Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi uliopita, kikosi cha Simba kinaanza mazoezi ya kuiwinda Lipuli leo.

Mazoezi yatafanyika Uwanja wa Boko Veterani baada ya timu kupewa mapumziko ya siku moja baada ya mchezo uliopita.

Simba itakuwa mgeni wa Lipuli FC katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Samora mjini Iringa Jumamosi ya Aprili 21 2018.

Wakati huohuo wapinzani wao katika mchezo huo wameweka wazi kuwa hawaiogopi Simba kwa chochote na kilichowakuta Singida United basi nao wajiandae.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.