Juuko Kuachana Na Simba..


Beki wa Simba, Juuko Murshid amesa licha ya kupata nafasi kadhaa kwenye kikosi cha klabu hiyo anahitaji kurejea nchini kwao(Uganda) ifikapo mwisho wa msimu huu.

Juuko amecheza mechi 20 msimu huu katika michuano yote ambayo Simba inashiriki msimu huu, ambapo katika michezo hiyo 16 ameaza katika kikosi cha kwanza na minne pekee akianzia benchi.

Juuko amesema kuwa anaamini kuwa kunakitu ameifanyia Simba  na alichostahili kufanya amekifanya na yupo tayari kuondoka nchini.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa simba ni klabu bora Afrika na anaweza sema kureje Simba "Ndio"  ngoja tuone hadi kumalizika kwa msimu huu.

Mkataba wa Juuko na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu huu na tayari klabu ya KCCA imeweka wazi nia ya kumnasa beki huyo.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.