Fainali ASFC(FA) Kufanyika Nje Ya Dar Huu Hapa Mkoa Itakapofanyika


Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza mchezo wa fainali ya kombe la FA utachezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha, Juni 2.

Kwa miaka mingi sasa mkoa wa Arusha umekosa mwakilishi katika ligi huku timu za JKT Oljoro, Madini FC na AFC Arusha zikiwa katika madaraja ya chini hivyo TFF imeamua kuwapelekea burudani hiyo msimu huu.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa fainali hizo kufanyika nje ya jiji la Dar es Salaam baada ya mwaka jana kupigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Michuano hiyo imefikia hatua ya nusu fainali ambapo timu za Singida United, Mtibwa Sugar, JKT Tanzania na Stand United zimetinga hatua hiyo.

Timu mbili kati ya nne tajwa hapo juu zitakutana katika mchezo wa fainali utakaopigwa dimbani hapo Juni 2.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.