NEYMAR KUREJEA UWANJANI MWEZI UJAO BAADA YA VIPIMO


Supastaa wa PSG, Neymar amesema anatarajia kurudi uwanjani baada ya kufanyiwa vipimo vya mwisho Mei 17.

Neymar yupo nje ya uwanja tangu mwezi Februari baada ya kuvunjika mguu huku mwenyewe akitarajia kurejea mapema.

Raia huyo wa Brazil amesema kuwa, "Inabidi niweke tarehe maalum ambayo ni Mei 17. Siku zote huwa nawasiliana na kocha wa Brazil Tite pamoja na mshauri wa ufundi, Edu Gaspar kuhusu hali yangu.

"Nimepata muda mzuri wa kurejea tayari kwa fainali za kombe la dunia, sio vizuri kupata majeraha lakini kwangu nimechukulia kama mapumziko," alisema Neymar.

Neymar ameongeza kuwa ameichukulia hali hiyo kama changamoto na anatarajia kurudi uwanjani akiwa na nguvu kama za awali kwakua ndio mara yake ya kwanza kufanyiwa upasuaji.

Nyota huyo wa Barcelona alisema kwa sasa anaweza kufanya mazoezi mepesi huku akiwa na hamu kubwa ya kucheza fainali za kombe la dunia baada ya kusubiri kwa miaka minne.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.