AKILIMALI:- MKWASA AMEYATAKA MWENYEWE



-Katibu wa Baraza la wazee wa klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali naye ametoa neno kuondoka kwa kocha wa Yanga, George Lwandamina na kujiunga na klabu ya Zesco United.

-Asubuhi ya leo mzee akilimali amesema
"Lwandamina ni kocha mzuri sana tukubali tu timu yangu imepoteza mtu sahihi, Yanga ilikuwa inamhitaji bado Lwandamina ila viongozi wa Yanga ndio wamesababisha yote haya"

"Katibu tumempigia kelele kila siku atangaze mchakato wa uchaguzi ili nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo ijazwe ila yupo kimya. Timu imekosa fedha za kujiendesha kwa sasa ila angekuwepo mwenyekiti angekuwa na yeye ana mawazo chanya ya kupata fedha"

"Wamevunja Katiba ya Yanga kwa matakwa yao wenyewe, matatizo ambayo yapo kwa sasa klabuni hapo yamesababishwa na viongozi waliopo kwa sasa kwa kukumbatia mambo wenyewe wamekuwa wasiri kila jambo ona sasa wanaumbuka"
Alisema Mzee Akilimali

-Mzee akilimali alipoulizwa swali yeye kama katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga inaisaidiaje klabu hiyo kwa sasa na matatizo ambayo yaliyopo mzee Akilimali alijibu

"Katibu atangaze mchakato wa kujaza nafasi iliyoachwa na Bwana Yusuph Manji iwapo wana Yanga watataka niwe mwenyekiti wa klabu hiyo nitaisaidia kwa moyo mmoja"

"Watu hawajui jina la Ibramovic limetoka wapi mimi sishindwi kuisaidia klabu ya Yanga kwa sasa ila nitaisaidiaje niko nje ya mfumo"

Alisema Akilimali kwa sauti ya upole.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.