Azam Yaendelea Kufanya Madudu VPL Yaanza Kujitoa Kwenye Mbio Za Ubingwa.
Ligi kuu Tanzania bara ambayo inaelekea ukingoni leo imeendelea kwa michezo kadhaa ya raundi ya 25 ya ligi hiyo ambapo kwa mujibu wa matokeo ya michezo hiyo klabu ya Azam imeendelea kufanya vibaya baada ya keo kushindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani na kutoa sare na timu ikiyoko mkiani mwa ligi hiyo, Njombe Mji.
Azam ambayo imekwenda katika mchezo huo ikwa na lengo la kuishusha Yanga kutoka katika nafasi ya pili na kuendelea kuifukuza Simba kimya kimya imeshindwa kuonyesha jitihada zake baada ya kutoka suluhu na Njombe mji na hivyo kugawana pointi moja kila mmoja.
Haya hapa matokeo kamili.
Aidha ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho kwa michexo kadhaa na hii hapa ratiba kamili.
Simba vs Tanzania Prisons,
Ndanda FC vs Ruvu Shooting,
Kagera Sugar vs Mtibwa Sugar.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.