Yanga Wamtangaza Mrithi Wa Lwandamina Rasmi.


Uongozi wa Yanga umemtangaza atakaekaimu nafasi ya kocha mkuu iliyoachwa wazi na George Lwandamina ambaye katikati ya juma hili alirejea kwao na kuijiunga na klabu yake ya zamani ZESCO united.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Katibu mkuu wa Yanga ni kuwa alikuwa kocha wa viubgo wa klabu hiyo, Noel Mwandila ndiye mrithi wa Lwandamina.
“Ambaye alikuwa kocha msaidizi Noel Mwandila amekuwa kaimu kocha mkuu kwa sababu mwalimu hayupo na timu haiwezi kuwa bila kocha mkuu kwa hiyo mkuu wa benchi la ufundi kwa sasa atakuwa Noel Mwandila akisaidiwa na Shadrack Nsajigwa.”

Aidha Katibu Mkwasa amesema kuwa uongozi wa Yanga umemwandika barua George Lwandamina kumuomba ajiunge na timu Ethiopia ambapo itakuwa ikicheza mchezo wa marudiano dhidi ya Wolaitta Dicha kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika.
“Tumejaribu kumjibu barua ya kujiuzulu lakini pia tumemwandikia kwamba bado tuna nia nae na akaungane na timu Ethiopia lakini bado hatujapata majibu na hatujajua ni kwa sababu gani lakini tumejitahidi hatujapata jibu sahihi.”
“Aliwasilisha barua ya kujiuzulu lakini barua lazima ikubaliwe, sisi tukajibu kwa sababu klabu bado ilikuwa na nia na huduma yake na ilikuwa imebaki miezi mitatu ni bora angemalizia lakini sasa kama masuala ya kutokujibu ni ya kwake. “

Mkwasa pia amekanusha taarifa kwamba yeye atarejea kwenye benchi la timu hiyo baada ya kuondoka kwa George Lwandamina.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.