Wapinzani wa Yanga waingia nchini


Kikosi cha wachezaji 21 wa timu ya soka ya Township Rollers ya Botswana pamoja na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Mserbia Nivola Kavazovic kimetua salama jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa raundi ya kwanza ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Dar Young Africans.


Township wanawasili nchini wakiwa wametoka kuchukua taji la 2018 Mascom Top 8 baada ya kuwafunga Orapa United kwa mabao 4-2 katika uwanja wa Francistown Sports Complex siku ya Jumamosi.


Ikumbukwe kabla ya kukutana na Yanga baada ya kuitoa timu ngumu ya Al Merreikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 4-2 katika mchezo wa hatua ya awali.


Wachezaji waliokuja


Mwampule Masule, Keagile Kgosipula na Wagarre Dikago, Walinzi ni Thato Bolweleng, Mosha Gaolaolwe, Simisani Mathumo, Tshepo Motlhabankwe, Kaone Vanderwesthuizen, Edwin Olerile na Percy More


Viungo ni Gape Mohutsiwa, Ivan Ntege, Ofentse Nato, Maano Ditshupo, Edwin Moalosi, Segolame Boy, Ntesang Simanyana, Galabgwe Moyana, Lemponye Tshireletso, Joel Mogorosi, Tshepo Matete, Motsholetsi Sikele, Boyo Lechaena na washambuliaji ni Bogosi Nfila na Mthokozisi Msomi.


Yanga na Towship Rollers watakutana siku ya Jumanne, Machi 6 2018 katika mchezo ambao utafanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Waamuzi wa mchezo

Waamuzi wa mchezo huo watatoka nchini Burundi ambapo Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Willy Habimana na mwamuzi msaidizi namba mbili Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo anatoka Swaziland ambaye ni Mangaluso Jabulani Langwenya


Mechi ya marudiano itachezwa Machin 17, 2018 nchini Botswana na itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.