Wapinzani Wa Yanga Klabu Bingwa Afrika (CCL) Kutua Nchini Kesho
Kikosi cha Township Rollers kinatarajiwa kuwasili kesho Jumapili, March 04 tayari kwa mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya mtoano dhidi ya mabingwa wa Tanzania, Yanga.
Mchezo huo utapigwa Jumanne, March 06 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Leo Rollers itashuka dimbani kucheza mchezo wa fainali michuano ya Mascom Top 8 dhidi ya Orapa United katika mji wa Francistown.
Tayari baadhi ya viongozi wa timu hiyo wako jijini Dar es salaam kwa siku kadhaa sasa wakiweka sawa mapokezi ya timu yao.
Yanga tayari iko jijini Dar es salaam ikiendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo ambao ushindi ni lazima ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Kama itafanikiwa kutinga hatua ya makundi, Yanga itajihakikishia kukamata kitita cha Tsh Bil 1.2.

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.