Azam FC waiijia Juu Kamati Ya Nidhamu Kufungiwa Kwa Razak Abalora.


Klabu ya Soka ya Azam imelalamikia kitendo cha Kamati ya Bodi ya Ligi ya Uendeshaji na Usimamizi ya Ligi kumsimamisha kipa wao, Razak Abalora hadi suala lake litakapotolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Azam imesema jambo hilo linatia ukakasi kwani kabla ya hukumu hiyo tayari Abalora ameshacheza zaidi ya michezo minne jambo ambalo linazidi kutia doa vyombo vya maamuzi ndani ya Shirikisho hilo.

"Uamuzi aina hii haupo kabisa kwenye soka la kisasa kwa vyombo vya uendeshaji wa ligi, mara kwa mara tumeshuhudia katika ligi za wenzetu wakichukua hatua kwa haraka ndani ya siku kadhaa kwa wachezaji wanaofanya vitendo vya utovu wa nidhamu," taarifa ya klabu hiyo imesema.

"Azam FC inaheshimu uwepo wa vyombo hivi, lakini tunachoomba ni lazima vifanye kazi yao kwa uharaka ili kuondoa viulizo kwenye maamuzi wanayochukua baada ya muda mrefu kupita tena taarifa nyingine zikitumwa usiku siku moja kabla kuelekea mchezo husika wa klabu," imesema.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.