Manara: Simba Na Yanga Sio Maadui Wala Sio Mahasimu Wa Jadi.


Afisa habari wa Simba sc, Haji Manara amesema kuwa vilabu vya Simba na Yanga sio maadau licha ya upinzani mkubwa ambao umekua ukijidhihilisha waziwazi kupitia kwa wapenzi, mashabiki, wachachama na hata viongozi wa vilabu hivi.

Kwa mujibu wa Manara ameeleza kuwa Yanga na Imba sio maafui bali niWatani wa Jadi aidha ameongeza kwa kusema kuwa hua analikataa jina la mahasimu wa jadi.


Guys nilichofundishwa mm Simba na Yanga c maadui ni watani wa jadi na ndio maana mm nalikataa jina la mahasimu wa jadi ambalo linatokana na neno Hasama,
Leo kwenye msiba wa mchezaji wetu wa zamani Arthur Mambeta sote tulishirikiana kikamilifu,pichani nikiwa na mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa Kitwana Manara ambae ni baba yangu mkubwa..picha nyingine nikiwa na katibu Mkuu wa Yanga na nyota wa zamani wa Timu hyo Charles Boniface Mkwasa pamoja na ex Chairman wetu Mzee Hassan Dalali @simbasctanzania @Yangasc 🙏🙏

Manara ameyasema hayo muda mfupi baada ya kupiga picha na baadhi ya viongozi wa Yanga ambao wamehudhuria msibani kwa aliekuwa mchezaji wa Simba marehemu mzee Arthur Mambeta..

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.