TFF Yamteua Nyamlani Kurithi Nafasi Ya Wambura.


Kamati tendaji cha shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) imemteua Athuman Nyamlani kuwa kaimu makamu wa Rais wa shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Nyamlani anachukua nafasi ya Michael Richard Wambura aliyefungiwa maisha na kamati ya maadili kutojihusisha na masula ya mpira.

Ingawa Michael Richard Wambura amekata rufaa katika kamati ya Rufaa ya TFF.

Kwa mujibu wa Kanuni na Taratibu za TFF mtu ambaye anatakiwa kukaimu nafasi ya Uongozi kwa nafasi ya kuchaguliwa anatakiwa kuwa mjumbe wa muda mrefu wa TFF ambaye yupo kwenye kamati tendaji.

Waliokuwa na sifa

Kwa wajumbe wa kamati tendaji ambao wana muda mrefu kwenye shirikisho kwa sasa ni watatu (Ahmed Mgoyi, Nyamlani na Khalid Mohamed) Kikao cha kamati tendaji kinachoendelea jijini Dar es Salaam kilishidwana kwenye kumpitisha Athuman Nyamlani kukaimu nafasi hiyo ndipo kura za Ndio na hapana zikapigwa na kura za Ndio zikawa nyingi akapitishwa Athuman Nyamlani kuwa kaimu Makamu wa Rais wa TFF mpaka pale mkutano mkuu utakavyoamua vingine.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.