Tambwe Kukosekana Mchezo Wa ASFC Dhidi Ya Singida United


Yanga inaweza ikawatumia kiungo Thabani Kamusoko na Mshambuliaji Donald Ngoma kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Singida United siku ya pasaka, April 01 mkoani Singida.

Ngoma na Kamusoko wamekuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kinachojifua mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo huo ambao mshindi ataukaribia ubingwa wa kombe la FA (ASFC) kwani atatinga hatua ya nusu fainali.

Aidha kumekuwa na matumaini makubwa kwa Ngoma aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu, kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga katika mchezo huo kwani amekuwa akifanya kikamilifu mazoezi yanayotolewa na kocha George Lwandamina.

Tambwe ameachwa jijini Dar es salaam kujiimarisha zaidi na ataungana na kikosi cha Yanga kitakaporejea baada ya mchezo dhidi ya Singida United.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.