Waachezaji wanne Yanga Waliokuwa na Stars Kuelekea Moro Mchana Huu Kabwili Abakia Dar Sababu Hii Hapa.


Wachezaji wa Yanga waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa mchana huu wanasafiri kuelekea Morogoro kuungana na wenzao tayari kwa mchezo wa ASFC dhidi ya Singida United.
Wachezaji hao ni Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael, Hassan Kessy Na Kelvin Yondani.

Aidhi goli kipa kinda wa klabu hiyo Ramadhani Kabwili yeye amebakia Dar es salaam kwa ajili ya kujiunga na wenzake wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes.

Yanga watashuka dimbani katika uwanja wa Namfua ulipo Singida kuwakabili wenyeji wao Singida United siku ya Jumapili Aprili mosi mwaka huu.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.