Huku Kwetu Mambo Ni Hivi Yanga Jipangeni.


Wakati ukingojewa mchezo wa Simba na Njombe kupigwa mnamo Aprili 3, klabu hiyo imeendelea na mazoezi ambayo yamekuwa yakifanyika katika uwanja wa Bocco veterani.

Katika mazoezi hayo kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima pamoja na Beki wa timu hiuo Salimu Mbonde wao wapo katika mazoezi mepesi ya wiki moja kabla ya kujumuishwa katika kikosi ili kufanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzao.

Aidha imeelezwa kuwa Niyonzima huenda asionekane dimbani akisakata kandanda kwenye mchezo huo ambapo imekuwa ikidaiwa kuwa anapikwa ili kuwakabili Yanga mnamo Aprili 29.

Niyonzima ambaye alikuwa nje ya uwanja muda mrefu hadi kufikia hatua ya kwenda India kwa ajili ya matibabu ya mguu, amepewa muda wa wiki moja kwa ajili ya mazoezi mepesi ya kujiweka fiti.

Kiungo huyo wa zamani wa Yanga alikuwa nje ya uwanja muda mrefu akisumbuliwa na majeraha ya mguu, amepewa muda huo na kocha wake mkuu, Pierre Lechantre ambaye hajamtumia tangu alipotua kikonoa kikosi hicho kutokana na hali hiyo ya kuwa majeruhi.

Mashabiki wengi wa Simba wana hamu ya kumuona Niyonzima akiwa uwanjani kabla ya mchezo dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga ambapo timu hizo zitakutana katika Ligi Kuu ya Vodacom mnamo Aprili 29, mwaka huu.

Mchezaji mwingine wa Simba ambaye alikuwa majeruhi kwa muda ni beki wa kati, Salim Mbonde, ambaye naye ameanza mazoezi sambamba na Niyonzima baada ya kutoka kwenye majeraha ya goti, kisha kupata ajali hali ambayo ilimfanya akae nje ya uwanja tangu Oktoba, mwaka jana.

Endapo wawili hao wakiwa fiti kwa muda huo waliopewa, wanaweza kuwa msaada katika kikosi cha Simba kuelekea mchezo huo wa Aprili 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa pamoja na michezo mingine ya kuwania ubingwa wa michuano hiyo.

Simba na Yanga zimeoangwa kukutana 29.04.2018 baada ya kupanguliwa ratiba iliyokuwa ikionyesha kuwa klabu hizo zingemenyana tarehe 07.04.2018.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.