Simba Waanza Mazoezi Rasmi..
Kikosi cha Simba kimeanza mazoezi leo Jumamosi kujiwinda na mchezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Njombe Mji.
Wachezaji wa Simba walipewa mapumziko ya wiki nzima Jumamosi iliyopita baada ya mchezo dhidi ya Al Masry uliomalizika kwa suluhu ya 0-0 na kuifanya Simba iondoshwe kwenye michuano ya kombe la Shirikisho.
Kikosi hicho kitakuwa ugenini kucheza mechi hiyo ya ligi Aprili 3 2018 katika Uwanja wa Sabasaba kabla ya kusafiri mkoani Morogoro kuivaa Mtibwa Sugar, April 08.
Benchi la Ufundi la Simba limeweka bayana kuwa watahakikisha Simba haifanyi makosa katika michezo 10 iliyobaki ili kuweza kutwaa ubingwa wa VPL msimu huu na hatimaye kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Kimataifa mwakani
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.