Robo Fainali Ya Azam Sports Fedaration(ASFC) Kuanza Kutimua Vumbi Leo, Hii Hapa Ratiba Kamili.
Hatua ya robo Fainali ya
Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC) inatarajia kuanza kutimua vumbi leo Ijumaa ya March 30-2018 kwa kupigwa mchezo mmoja tu.
Leo Ijumaa ya March 30-2018, utapigwa mchezo mmoja wa robo Fainali, ambapo Stand United 'chama la wana' itakuwa ina kibarua dhidi ya Njombe Mji katika Uwanja wake wa nyumbani wa CCM Kambarage.
Mchezo huo ambao ndio wa kwanza katika michuano hii hatua ya robo Fainali unatarajiwa kupigwa majira ya saa 16:00 jioni.
Mshindi wa mchezo huu atakwenda moja kwa moja Nusu Fainali, ambapo atakutana na mshindi kati ya Azam Fc vs Mtibwa Sugar wanaocheza hapo kesho Jumamosi ya March 30-2018.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.