Lipuli Mambo Ni Hivi Kuelekea Mchezo Dhidi Ya Mbao Fc.


Timu ya Lipuli Fc imemeendelea na maandalizi ya mwendelezo wa ligi kuu Tanzania bara ambayo kwa sasa imesimama kwa muda kupisha mechi za kalenda ya FIFA.

Katika kuelekea mchezo ujao wa ligi hiyo ambao utawakutanisha Lipuli na Mbao afisa habari wa klabu hiyo Clement Sanga ameueleza mtandao wa "sokakiganjani.blogspot.com" kuwa klabu hiyo inaendelea vyema na mazoezi kwa awamu mbili kila siku.

Sanga amesema klabu hiyo imekuwa ikifanya mazoezi asubuhi na jioni na kwa jana asubuhi Lipuli ilifanya mazoezi katika uwanja wa Kichangani na jioninkifanyia katika uwanja wa Samora.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa leo klabu hiyo haitakuwa na mazoezi ya asubuhi badala yake itafanya mazoezi ya jioni katika uwanja wa chuo kikuu cha Mkwawa kilichopo Iringa.

Hali za wachezaji.

Kuhusu maendeleo ya wachezaji msemaji huyo amesema wachezaji wote wapo katika hali nzuri na hakuna majeruhi katika timu hiyo.

Zaidi zaidi amesema kuwa licha ya kutokuwa na mchezo wa kirafiki katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama ila wanaamini watafanya vizuri katika michezo ijayo.

Mwisho amewaomba mashabiko wa klabubhiyo kuiunga mkono klabu hiyo bila kukata tamaa ili kuhakikisha inafanya vizuri katika michezo yake yote.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.