PICHA: TRAINING YA DR. CHRIS MAUKI KUHUSU SELF-CONFIDENCE KWA WACHEZAJI WA KLABU YA SIMBA: SEA SCAPE HOTEL: 04.03.2018
Daktari na Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia, Chris Mauki, ametoa somo kwa wachezaji wa Simba katika Hotel ya Sea Scape iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mauki ametoa somo la namna ya mchezaji anapaswa kujijengea ujasili pale anapokuwa ndani ya uwanja.
Mtaalamu huyo ameeleza namna mchezaji anapaswa kujitambua na kujiamini pindi anapokuwa uwanjani wakati wa mechi ili kuisaidia timu kupata matokeo chanya.
Somo hilo kwa wachezaji wa Simba limekuja kufuatia maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya A Masry SC utakaopigwa Jumatano ya wiki hii Uwanja wa Taifa.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.