Pambazuka Na Habari Njema Kutoka Yanga Asubuhi Ya Leo.


Kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kuendelea na mazoezi baada ya mapumziko ya siku kadhaa ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo wa kombe la FA dhidi ya Singida United utakaopigwa kwenye uwanja wa Namfua April 01.

Baadhi ya wachezaji walio na majukumu na kikosi cha timu ya Taifa ambao ni Ramadhani Kabwili, Hassani Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani na Ibrahim Ajib wataendelea kukosekana hadi baada ya mchezo wa Stars dhidi ya DR Congo.

Stars itacheza na DR Congo kesho Jumann March 27 katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Habari njema kwa kikosi cha Yanga ni kwamba sasa hakuna majeruhi wachezaji wote wakiwemo Amissi Tambwe, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Yohana Nkomola wamerejea kikamilifu kujifua na wenzao baada ya kumaliza program binafsi za mazoezi.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.