Niyonzima Arejea Kuteka Akili Za Lechantre Na Djuma.


Kiungo wa klabu ya Simba, Haruna Niyonzima ameanza mazoezi na wachezaji wenzake rasmi mara baada ya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu zaidi wakati akiuguza majeraha yake.

Niyonzima ambaye hivi karibuni alitangaza kurejea dimbani huku akishuhudiwa akifanya mazoezi binafsi ili kuhakikisha anauweka sawa mwili wake ili kumrahisihia kufanya vyema kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara..

Aidha kiungo huyo mwenye uraia wa nchi ya Rwanda amesema atafanya juu chini kuhakikisha anamwaminisha kocha Lechantre na msaidizi wake Masoud Djuma  ili wampatue nafasi kwenye kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa awali.

Niyonzima alionekana jioni ya jana akifanya mazoezi katika uwanja wa Bocco veterani ili kujiandaa na michezo mbalimbali..

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.