Simba yaiwekea Mtibwa Kambi baada ya kuwanyuka Njombe Mji.


SIMBA SC imeondoka Njombe leo asubuhi kurejea Iringa kuweka kambi ya siku mbili kabla ya kwenda Morogoro kwa mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Jumatatu ijayo.

Simba SC jana ilijitanua kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Njombe Mji FC Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.
Pongezi kwa mfungaji wa mabao hayo yote mawili leo, Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’, moja kila kipindi na sasa Wekundi wa Msimbazi wanafikisha pointi 49 baada ya kucheza mechi 21, wakiwazidi kwa pointi tatu mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 43 za mechi 21 pia.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa chipukizi Meschak Sudakutoka Songea, aliyesaidiwa na Mohamed Mkono wa Tanga, Bocco alifunga bao la kwanza dakika ya 17 na la pili dakika ya 64.
Ikumbukwe Simba ilikwenda Njombe ikitokea Iringa pia ambako iliweka kambi ya siku mbili kabla ya mchezo huo na leo wanarudi tena mkoani humo kujiandaa na mchezo huo.
Wekundu wa Msimbazi, wamepania kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 ili kurejesha heshima yao.


Join us on WHATSAPP
 Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.