MO IBRAHIM AIANGUKIA SIMBA SC
-Baada ya Kocha mkuu wa klabu ya Simba, Mfaransa Pierre Lenchantre kumlalamikia Kiungo wa klabu hiyo Mohamed Ibrahim kwa utovu wa nidhamu wa kusingia ana matatizo ya Kifamilia na kutoenda mazoezini na kuifanya klabu hiyo kama klabu ya sikukuu
-Kocha wa klabu hiyo alisema hataweza kumtumia kiungo huyo kwa sasa ndani ya kikosi cha Simba kwa sababu ya kutofanya mazoezi na wachezaji wenzake kwani alikuwa anakosa mazoezi ya timu kila mara kwa kusingizia ana matatizo ya Kifamilia.
-Baada ya Malalamiko hayo kuyapata kiungo Mohamed Ibrahim 'Mo' ameenda kwa uongozi wa klabu hiyo na kuuangukia na kuomba msamaha ili umsamehe yeye ni binadamu amekosea wamusamehe na yupo tayari kurejea kazini kufanya kazi kuanzia sasa.
-Uongozi wa Simba kupitia kwa Kaimu Rais wa klabu hiyo Salim Abdallah "Try Again" wameamua kumsamehe Mohamed Ibrahimu maarufu kama Mo na kusainishana makubaliano Maalumu ya kutorudia tena utovu wa nidhamu huo. Pia Mo amewaomba viongozi wa Simba wakamuombee msamaha kwa bechi la Ufundi la klabu hiyo
-Rais wa klabu hiyo wamepanga kesho ataongozana na Mohamed Ibrahim kwenda kuonana na bechi la ufundi la klabu hiyo likiongozwa na mfaransa Pierre Lechantre akisaidiwa na Masoud Djuma kama kocha msaidizi, Mohamed Aymen Hbib kocha wa viungo, Muharam Mohamed kocha wa makipa kuliomba msamaha ili arejee kazini.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.