MAKALA: KONA YA MOJA KWA MOJA


Na Zaka Zakazi

Kumbukumbu zangu zinanionesha kwamba Aishi Manula anakuwa kipa wa tatu wa Simba SC kufungwa kwa kona ya moja kwa moja.

1. IDD PAZI -1986

-alifungwa na beki wa kushoto wa Tukuyu Stars ya Mbeya, Daniel Chundu, kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi ikaisha kwa sare ya 1-1...Tukuyu Stars walitwaa ubingwa msimu huo.

2. MOHAMED MWAMEJA - 1996

-Ilikuwa dhidi El Mokawloon, maarufu kama Arab Contractors ya Misri, kwenye mchezo wa raundi ya awali ya Kombe la CAF (ambalo mwaka 2004 liliunganishwa na Kombe la Washindi na kuzaa Kombe la Shirikisho).

Katika mchezo wa kwanza hapa nyumbani, Simba walishinda 3-1 hivyo kuhitaji sare yoyote ili watinge raundi ya kwanza, wakaishia kufungwa 2-0 na kutolewa kwa sheria ya bao la ugenini.

Wakiwa nyuma kwa 1-0, beki wa Simba, Mathias Mulumba, akashinda mpira ndani ya eneo la hatari na kuwa penati. Mohamed Mwameja akaiokoa na kuwa kona ambayo ilipigwa na kuingia moja kwa moja.

3. AISHI MANULA - 2018
-Ni Aaron Lulambo wa Stand United aliyemshangaza 'Tanzania One' Aishi Manula kwa bao la kona ya moja kwa moja, katika mchezo wa raundi ya 20 ya ligi kuu msimu wa 2017/18 ambapo vinara Simba walilazimishwa sare ya 3-3.

Lakini Aishi pia anafungwa bao la pili la kona ya moja kwa moja. Alipokuwa Azam FC, alifungwa Hood Mayanja wa African Lyon kwenye mchezo wa kwanza wa msimu wa 2016/17 dimbani Azam Complex Chaamazi.

Makipa wengine waliowahi kufungwa kwa kona ya moja kwa moja.

Ali Mustapher Mtinge 'Barthez' wa Yanga aliyefungwa Shiza Kichuya wa Simba msimu wa 2016/17. Mechi iliisha kwa sare ya 1-1.

Razak Abalora wa Azam FC aliyefungwa na Marcel Boniventure Kaheza wa Majimaji FC msimu huu. Mechi iliisha kwa sare ya 1-1.

Kipa wa Lipuli aliyefungwa na William Lucian 'Gallas' wa Ndanda. Mechi iliisha kwa sare ya 2-2.( Kwasi Asante alifunga bao kwenye mchezo huu, kama ilivyokuwa dhidi ya Stand United).

Nikumbushe makipa wengine wa hapa nyumbani unaowajua...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.