Lwandamina Ndio Basi Tena Yanga..


BAADA ya kuwepo taarifa kuwa huenda Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina akatimkia katika Klabu ya Zesco, uongozi wa Yanga umefunguka na kuzungumzia mkataba wa kocha huyo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amefunguka kuwa licha ya kuwa mkataba wake unaelekea ukingoni, hawawezi kumzuia kocha huyo kuondoka.

Kocha huyo mpaka sasa amebakiza miezi michache ndani ya klabu hiyo ili kumaliza mkataba wake Juni, mwaka huu.

“Habari hizo za kocha kwenda Zesco na mimi nasikia na kuona mitandaoni lakini kikubwa ninachofahamu ni kwamba kocha yupo na sisi na mkataba wake unamalizika mwezi wa sita mwaka huu.

“Lakini pia sisi kama klabu hatuwezi kumzuia kuondoka kama kuna klabu inamhitaji au timu fulani imempa ofa kama ipo, hivyo atatujulisha huenda labda amepata maslahi mazuri zaidi ya hapa, japo hajasema lolote.

“Na pia sisi kama klabu tuna imani naye kuendelea kufanya kazi, hatuna tatizo naye, kama ni suala la kuondoka, hilo lipo mikononi mwake, hatuwezi kumsemea lakini klabu inamhitaji kuendelea kufanya kazi,” alisema

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.