MAYANGA ANAJITOLEA MWISHO JUMANNE.



-Kocha wa kikosi cha Taifa Stars, Salum Mayanga anajitolea kukinoa kikosi cha Tanzania, Taifa Stars baada ya mkataba wake kuisha January mosi mwaka huu.

-Mayanga alisaini mkataba wa mwaka mmoja January 01 mwaka jana kuifundisha Taifa Stars akichukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Boniface Chalres Mkwasa.

-Mpaka sasa Kocha Salum Mayanga ameiongoza timu ya Taifa katika michezo 14 amefanikiwa kushinda michezo 5 ametoa sare michezo 7 na amefungwa michezo 2 tu na mchezo wa jumanne ambao ni wa mwisho kwake kuifundisha Taifa Stars utakuwa mchezo wa 15.

-TFF iliachana na Mayanga tangu January 02 baada ya mkataba wake kuisha january 01 na sasa hivi walimuuita kwa maombi maalumu kuja kusaidia tu (kujitolea) kwa michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Algeria iliyochezwa alhamisi iliyopita tukafungwa (4-1) na hiyo ya Jumanne dhidi ya DRC Congo katika dimba la taifa.

-TFF wameanza mchakato tayari wa kumtafuta anakayechukua mikoba ya Salum Mayanga na mwezi ujayo ishu itakuwa hadharani mwezi ujao kwa majina ya waliotuma maombi kuwekwa wazi na kupelekwa kwenye kamati ya Ufundi ya TFF kupitia CV hizo ili kuchagua atakayefaa kuchukua mikoba ya Mayanga.

-TFF imepanga kuajiri kocha kutoka nje baada ya kuajiri makocha wazalendo wa miaka miwili bila mafanikio yoyote na kocha ambaye atamsaidia kocha atakayeajiriwa atakuwa Hemed Morocco ambaye anatoka Zanzibar.

@yossima Sitta Jr.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.