MANDAWA AZIDI KUTISHA BOTSWANA

Tokeo la picha la RASHIDI MANDAWA

MSHAMBULIAJI Mtanzania, Rashid Yussuf Mandawa anayechezea klabu ya BDF XI amekuwa tishio katika Ligi Kuu ya Botswana kutoka  na kasi yake ya kufunga mabao.
Straika huyo amekuwa kipenzi cha mashabiki wa soka nchini humo hasa wa klabu yake, aliyoifungia mabao 11 ambayo ni muhimu na ya kutosha msimu huu.
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online kwa simu kutoka Gaborone jana, Mandawa aliyesajiliwa timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, amesema anahitaji kusaidia timu yake kufanya vizuri na kupata tuzo ya mfungaji bora.


Katika msimamo wa wafungaji , Mandawa yupo nafasi 4 kwa mabao 11, nafasi ya ya tatu ni Tumisang Orebonye akitikisa wavu mara 12, wanaongoza ni Thatayaone Kgamanyane, Orebotse Mongae kwa mabao 13 na Kekaetswe Moloi anashika nafasi ya tano akiwa amefunga mabao 10.
Alisema hana hofu juu ya walimpita kwa idadi ya ufungaji akiamini atafikia idadi yao na  pita. 
"Lengo langu kusaidia timu yangu kufanya vizuri pamoja na kutwaa tuzo ya mfungaji bora," alisema.
Mandawa alisema anaimani ya kufikia idadi hiyo na kupita katika mechi moja au mbili.
"Kama nilifanikiwa kufunga hat trick katika mchezo na Township Rollers katika ligi nina imani katika mechi zinazokuja tutafanya vizuri na kufunga bao, alisema Mandawa.



Join us on WHATSAPP
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.