Manara:- "Kipindi cha mashaka kimewadia"


Afisa Habari wa Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kuwataka mashabiki wa wekundu wa msimbazi popote walipo Jijini Dar es Salaam wajitokeza kuenda kuwapa msaada kuwaokoa Yanga SC kufuatia mvua zinazoanza kunyesha.

Manara ametoa kauli hiyo ikiwa ni mzaha unaoendana na hali halisi ya uwanja wa wanajangwani uliyoopo katika bonde la Jangwani ambapo mvua ikinyesha eneo lote linageuka na kuwa bahari huku baadhi ya wakazi wa maeneo hayo hupelekea mpaka kupoteza mali zao, kubomokewa nyumba na kukosa mahali pa kulala.

"Kipindi cha mashaka kimewadia, 'always' nawaambia soka si uadui. Wanamsimbazi popote mlipo hapa Dar es Salaam, twendeni tukaokoe jamaa zetu tusiwaachie kitengo cha maafa pekee....Mvua ni kubwa na inahatarisha uhai na mali za wakazi wa mabondeni", amesema Manara.

Hali ya hewa ya leo Alhamisi katika Jiji la Dar es Salaam lilozoeleka kuwa na joto kali siku zote , limekuwa la tofauti baada ya kubarikiwa mvua tokea alfajiri katika baadhi ya maeneo.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.