Lipuli Kamili Kuawavaa Majimaji Fc, Wenyewe Walia Na Uwanja..
Mara baada ya kuwasili mjini Songea timu ya Lipuli leo imefanaya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa majimaji ikiwa ni siku moja kabla ya kuelekea kwenye pambano lake dhidi ya Majimaji fc linalotarajiwa kupigwa kesgo jumapili katika uwanja huo.
Maandalizi Ya Kikosi
Baada ya mazoezi Afisa habari wa klabu hiyo ya 'Wanapaluhengo' , Cement Sanga, amesema kuwa maandalizi yamekamilika na timu ipo tayari kwa mchezo wa kesho .
"TIMU IMEJIANDAA KWA MAZOEZI MAALUMU YA KUKABILIANA NA UKUUKUU WA HALI YA UWANJA NA IPO TAYARI KUIVAA MAJIMAJI HAPO KESHO HIVYOHIVYO.
Yaliyojiri Mazoezini
Hata hivyo kunataarifa zisizokuwa nzuri kwa Wanapaluhengo hao kwani mchezaji wake mmoja amepata majeraha baada ya kugonana na mlinda mlango lakini kwa mujibu wa Sanga hali yake ni nzuri.
"KTK MAZOEZI YA LEO MSHAMBULIAJI WETU MMOJA ADAM SALAMBA AMEPATA MAJERAHA BAADA YA KUGONGANA NA GOLIKIPA AGANTON MKWANDO NA KUUMIA KTK PAJA LAKE LA MGUU WA KUSHOTO. AMEPATIWA MATIBABU NA DAKTARI WA TIMU AMESEMA ANAWEZA KUCHEZA KESHO INATEGEMEA JERAHA LAKE LITAPONA HARAKA KWA KIASI GANI. TUNAOMBA MASHABIKI WETU WATUOMBEE TUPATE ALAMA TATU ZA KESHO DHIDI YA MAJIMAJI."
Hali Ya Uwanja
Aidha Sanga ameongeza kwa kusema kuwa hali ya uwanja hairidhishi na hii ni kutokana na miundombinu kuwa mibovu na kutoruhusu maji kutoka nje.
"TIMU IMEMALIZA MAZOEZI KTK UWANJA WA MAJIMAJI MJINI SONGEA LAKINI HALI YA UWANJA SIO NZURI SANA KWA VILE UMELOWA SANA BAADA YA MVUA KUNYESHA NA HAUNA MIUNDOMBINU MIZURI YA KUTOA MAJI NJE. UWANJA KWA KWELI SIO MZURI SANA. "
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.