Kumbe Simba Hawana Masihara Katika Suala La Uwanja Soma Hapa Kujua Zaidi...

Kaimu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah amesema kwamba mchakato wa kuzikomboa nyasi zake zilizokwama bandari utakamilika mwezi huu na mwezi ujao ujenzi utaanza hususani katika pitch.

"Tumejipanga, hili la Uwanja wa Bunju, na hadi kufikia mwisho wa mwezi huu, tutazikomboa nyasi za Uwanja wa Bunju ambazo ziko bandarini hadi sasa.

"Kuna mfadhili amekubali kutujengea uwanja na hili zaidi itakuwa uwanja wa kuchezea na kama uwanja una mambo mengi, suala hili hadi mwisho wa mwaka Simba inaweza kuwa katika hatua nzuri.

"Kingine ni kujenga ofisi za kisasa, Simba inataka kwenda na mabadiliko, itakuwa na ofisi za kisasa kabisa, na tunataka kuwa na chumba maalumu cha wanahabari, media centre kwamba habari zitakuwa zinarushwa kutoka klabuni.

"Hapa itakuwa kila kiongozi anapatikana hapo," alisema Salim bila kutaja eneo litakalojengwa ofisi za Simba.

Pia alisema uongozi wa Simba unafanya mpango wa kusafirisha mashabiki wake kwenda kuishabikia timu hiyo Misri ambapo tayari wameanza mazungumzo na uongozi wa ndege yenye uwezo wa kubeba watu 98.

Aidha kiongzo huo wa Simba alisema wanatarajia kufanya uhakiki wa wanachama wake ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika Mei mwaka huu

Vilevile Simba imesema kwamba inatarajia kuanzisha mchakato wa kadi mpya ili kuhakiki wanachama wake na ambao hawatalipia kadi watasitishwa uanachama wao.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.