Viingilio Kuziona Yanga Na Township Rollers.
Yanga inashuka uwanja wa Taifa keshokutwa Jumanne March 06 kuikabili Township Rollers, mabingwa Botswana kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika, raundi ya kwanza.
Yanga inayowakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo itaweza kutinga hatua ya makundi kama itavuka kigingi cha Township Rollers hivyo nguvu ya mashabiki wote inahitajika uwanja wa Taifa siku hiyo ya mchezo.
Mchezo unatarajiwa kuanza saa 10:30 jioni ili kuwapa nafasi mashabiki wengi hasa wale wanaotoka makazini kuwahi uwanjani.
Viingilio vya mchezo huo viko hivi;
VIP A - Tsh 20,000/-
VIP B na C - Tsh 10,000/-
Mzunguuko - Tsh 5,000/-
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.