Kocha Aliyefungiwa Kujihusisha Na Soka Miaka Mitano (5) Atoa Msimamo Wake ..
Mwalimu wa soka, 'Joseph Kanakamfumu' ambay hivi karibuni kamati ya Maadili ya TFF ilimuhukumu kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka 5 kutokana na tuhuma za kutoa taarifa zisizo sahihi na kughushi leseni za usajili.
Baada ya ukimya wa muda wa takriban saa 72 hatimaye kocha huyo ametoa msimamo wake kutokana na tuhuma hizo na kueleza kuwa atakata rufaa kutokana na maamuzi hayo.
"Habari za usiku huu wana michezo! Nillikuwa kimya kidogo toka juzi nikitafakari yaliyotokea dhidi yangu! Nikijiuliza nichukue hatua gani au niache tu! .Lakini dhamira imenishauri nisafishe jina langu, lakini kikubwa niangalie hatua za kufanya! Kubwa ni kukata Rufaa siyo kuomba Review sababu Review itasikilizwa na wale wale! Hivyo nimeweka kusudio la kukata rufaa baada ya taratibu Fulani za kisheria zitakapokamilika nikiambatanisha na fee ya Milioni moja"
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.