HABARI KUBWA KATIKA SOKA TANZANIA LEO IJUMAA.


Tokeo la picha la SOKA TANZANIA
Simanzi nchini Msiba mzito wa gwiji wa soka nchini na Mchezaji wa Zamani wa Simba Sc na timu ya Taifa ya Tanzania, Ather Mambeta alieyefariki jana Watanzania wamlilia familia yake yatoa neno sasa kuzikwa Jumamosi hiii Pumzika kwa amani .


Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Tanzania klabu ya soka Yanga jana wamewasili salama wakitokea mtwara akizungumza na wanahabari Mkwasa amesema vijana wako katika hali nzuri sasa wanajiandaa kuchezwa mchezo wa klabu bingwa barani Afrika.



Mnyama Simba fiti kuwavaa Stend united leo kuelekea mchezo uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa msemaji wao Haji s manara amesema kuwa kila kitu kipo sawa vijina wanakwenda kupambana huku wakiwa katika morali ya kupata matokeo katika mchezo wa leo.


Kocha Bilo nimekuja Dar kupambana na Simba sio kushangaa magorofa akizungumza na Sokaplace bilo amesema kuwa hali ya kikosi chake kipo safi hakuna amheruhi katika timu yao Bilo amesema kuwa wanaiheshimu Simba ila wataingia kupambana kupata point 3


Njombe mji Masau bwire huwezi kutupapasa lazima uache point 3 Njombe, Uongozi wa klabu ya soka ya Njombe mji umesema kuwa wamejipanga vyema kuelekea mchezo wa hapo kesho dhidi ya Ruvu shooting Huku wakisema kuwa wamemalizana na vijana wao wote wenye matatizo na Njombe mji imesema kuwa itaingia uwanjani kupigana kupata point tatu hapo kesho .


Raisi wa shirikisho la soka nchini Walice Karia amesema katika utawala wake atahakikisha anasimamia haki na misingi bora ya soka , karia amesema kuwa lazima tuweke mkakati ili kuipeleka mbali Tanzania katika mafanikio ya soka .


Lwandamina "nashangazwa na watu kuripo kuwa naondoka Yanga " Kocha huyo amesema kuwa kwa sasa bado ni mwajiriwa wa klabu ya soka ya Yanga hii ni baada ya mitandao ya kijamii kuandika kuwa Kocha huyo ataachana na Mabingwa watetezi wa ligi kuu Nchini Tanzania .


Ligi Kuu ya wanawake nchini Tanzania imeendelea jana kwa kupigwa mchezo mmoja, Mchezo huo uliwakutananisha Simba qeens dhidi ya mlandizi qeens mchezo huo ulimazika kwa Mlandizi qeens kugawa dozi ya goli nne kwa bila hapo jana .

Baada ya kuandaa vyema mkutano wa FIFa hapa nchini Tanzania Shirikisho la soka nchini Tff limepongezwa na shirikisho la soka duniani kwa matayarisho mazuri waliyofanya nasisi sokaplace tuwapongeze Serikali yetu kwa kuupokea vyema ugeni huo mkubwa nchini Pamoja na Tff kwa kufanya kazi nzuri .

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.