Yanga Yaipania Township Rollers..
Kikosi cha Yanga kimerejea jana kutoka mkoani Mtwara kukamilisha mzunguuko wa 19 ligi kuu ya Vodacom na kuibuka kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ndanda FC.
Yanga tayari imeanza mawindo yake kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers, Jumanne ijayo, March 06.
Akizungumzia maandalizi ya kuelekea mchezo huo, kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema ushindi walioupata Mtwara umeongeza morali ya wachezaji na sasa watachohitaji ni ushindi siku ya Jumanne.
Nsajigwa amesema benchi la Ufundi litatumia siku tatu zilizobaki kuelekea mchezo huo, kuweka sawa kikosi pamoja na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza kwenye michezo iliyopita.
Yanga ina dakika 180 kujaribu kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika, na kama itaibuka na ushindi mnono kwenye mchezo wake wa kwanza, inaweza kufanikiwa kutinga hatua hiyo kama itaweza kuepuka kipigo kwenye mchezo wa marudiano siku 10 baadae nchini Botswana.
Wachezaji Juma Mahadhi ambaye alikuwa anasumbuliwa na malaria, Thabani Kamusoko, Obrey Chirwa na Andrew Vicent Chikupe ambao walikuwa majeruhi ni sehemu ya wachezaji walioingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Township Rollers
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.