DONDOO ZA SOKA NA TETESI ZA USAJILI ULAYA LEO IJUMAA



Neymar awasili Brazil tayari kwa kufanyiwa Upasuaji wa mguu wake huku hofu ikitanda kwawapenzi wa klabu ya soka ya Psg kutoka na kumkosa nyota huyo kwa kipindi cha miezi mitatu .



Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Manchester city jana amefikisha mchezo wa mia moja kama kocha mkuu wa klabu ya Manchester city  huku mwaka huu huenda ukawa mwaka wamafanikio kwake .



Barcelona hoi yapata sare ya sita msimu huu ugenini dhidi ya lapalmas hapo jana usiki baada ya kupata sare ya goli moja kwa moja katika mchezo ambao ulikua wa kuvutia sana  Barcelona bado wanaongoza ligi wakiwa napoint zao 66.



Arsenal sikio lakufa halisikii dawa yapokea kichapo tena   cha goli 3-0 kutoka kwa Vinara wa ligi kuu nchini England klabu ya soka ya Manchester city jana usiku Magoli ya Manchester  city yamefungwa na Bernaldo silva , David silva pamoja na sane kwa mtokeo hayo bado Manchester city wapo kileleniwakiwa na point zao 75  huku  Arsenal  wapo nafasi ya 6 wakiwa napoint  45.





TETESI ZA SOKA MAJUU
Klabu za  Ligi kuu nchini England Liverpool na Totenham zimehusishwa kuwinda saini ya Mchezaji wa klabu ya soka ya Borrusia Dortmund Marco Reus  katika majira ya Kiangazi .



Klabu ya Arsenal imesema kuwa itasajili wachezaji watatu wa bei rahisi   msimu ujao  huku john evance akiwa akiwa chaguo namba moja kwao .




Vilabu ya Juventus Real madrid vimehusishwa kuwinda saini ya Mchezaji wa klabu ya Liverpool  Emre Can katika majira ya Kiangazi .



Klabu za Manchester united pamoja na Liverpool  zimehusishwa  kuwinda saini  kiungo mkabaji Victor wanyama Raia wa kenya  katika Majira ya kiangazi .




Wakala mino raiola amesema kuwa lazima mteja wake Gianluigi Donnarumma anayekipiga katika klabu ya Ac milan  aondoke katika majira ya kiangazi .



Nyota wa klabu ya soka ya Real madrid Christian Ronaldo amesema kuwa Real madrid iachane na kuwinda saini ya Harry kane badala yake imsajili mchezaji kutoka Bayernmunich
Robert Lewandowski   katika majira ya joto .



Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa  kocha mkuu wa Arsenal Wenger.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.