Emmanuel Okwi atangaza vita kali

Nyota wa klabu ya Simba Emmanuel Okwi amefunguka na kuitangazia vita kali wapizani wao Al Masry kuwa watapambana nao nguvu kwa nguvu waweze kuwafunga ili kusudi timu yake iweze kusonga mbele.
 
Okwi ametoa kauli hiyo akiwa katika kiwanja cha kufanyia mazoezi kwaajili ya kuweka sawa viungo kuelekea mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Masry unaotarajiwa kuchezwa kesho (Machi 16, 2018) Port Side nchini Misri.

"Mimi sipendi sana kutumia kutazama wapinzani wetu kitu gani wanachofanya kwasababu hiyo mimi sio kazi yangu, kinachonihusu mimi ni kuangalia timu yangu na safu ya wacheza wenzangu kuwa tupo vizuri katika kupambana. Al Masry ni timu ambayo tunaiheshimu lakini hatuwaogopi tutahakikisha tutapambana nao nguvu kwa nguvu ili mwisho wa siku timu ambayo itamzidi mwenzake ujanja iweze kuendelea mbele", amesema Okwi.
Pamoja na hayo, Emanuel Okwi ameendelea kwa kusema "sijali kama wapinzani wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika wananitazama sana ama laa lakini ninachowaza ni kupambana ili timu yangu isonge mbele".
Kwa upande mwingine, Emmanuel Okwi amesema anategemea kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wenzake pindi watakapoingia dimbani ili aweze kuipatia magoli timu yake ya Simba.



Join us on WHATSAPP
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.