Dismas Ten: "Ni muhimu kujua umuhimu wa kushinda mechi za nyumbani kwenye mashindano ya kimataifa"


Afisa habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten amesema kuwa ni muhimu kutambua umuhimu wa kupata matikeo katika viwanja vya nyumbani kuliko kutegemea kufanya mapinduzi kwenye viwanja vya ugenini.

Kauli hiyo ameisema leo mchana ambapo alikua akizungumza na wanahabari katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika majira ya saa nane mchana.

"Ni muhimu kujua umuhimu wa kushinda mechi za nyumbani kwenye mashindano ya kimataifa,tumerudi kwenye kombe la shirikisho baada ya kutokufanya vizuri ligi ya Mabingwa,maandalizi yanaaza sasa kuhakikisha tunafanya vizuri " -Dismas Ten.

Kauli hiyo ya Dismas Ten imekuja baada ya klabu hiyo kuondolea kunako michuano ya klabu bingwa Afrika na klabu ya Township Rollers baada ya kukubali kupokea kipigo cha goli 2-1 katika uwanja wake wa nyumbani na kushindwa kusawazisha kunako uwanja wa ugenini.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.