Azam Fc Yazidi Kujifua Bila Nyota Wake Watatu Akiwemo Nahodha, Himidi Mao
Kikosi cha Klabu Azam FC, jioni ya jana kilifanya mazoezi bila kuwa na nyota wake watatu akiwemo nahodha Himid Mao 'Ninja', Shaaban Idd na Yahya Zayd, ambao ni miongoni mwa nyota walioitwa kwenye kikosi kipya cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', kitakachocheza mechi mbili za Kimataifa za kirafiki zilizo katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) mwezi huu.
Kikosi hicho kipo katika maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utakuwa ni mchezo wa robo fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup.
Stars itaanza kukipiga na Algeria ‘The Green’ Machi 22 ugenini jijini Algiers kabla ya kurejea nyumbani, Dar es Salaam kuwakaribisha DR Congo ‘The Leopards’ Machi 27 kwenye Uwanja wa Taifa.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.