Makocha Mapacha Wa Al-masry Waongezewa Mkataba Baada Ya Kuwaondoa Simba Sc..


Bodi ya klabu ya Al-masry imewaongezea mkataba wa miaka minne makocha wa klabu hiyo  mapacha, Hossam Hassan na Ibrahim Hassan wa kuendelea kuinoa klabu hiyo kwa misimu minne mingine.

Maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha dharura kati ya Mapacha hao na uongozi wa bodi hiyo kilichofanyika mara baada ya mchezo dhidi ya Simba sc uliomalizika kwa sare tasa.

Katika hatua nyingine klabu hiyo hapo jana imeazimisha miaka 98 tangu kuanzishwa kwake huku ikijivunia mafanikio makubwa ambayo imeyapata kwa kipindi chote.

Hata hivyo baada ya shamrashamra za kuiondoa Simba katika michuano ya kombe la Shirikisho na maazimisho hayo ya miaka 98 klabu hiyo imetoa mapumziko ya siku mbili yaani jumapili na jumatatu na hivyo timu itarejea kambini kesho jummanne.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.