Amri Kiemba Na Thomas Maurice Watundika daluga Rasmi..
Amri Kiemba na Thomas Maurice leo Jumamosi Machi 24, 2018 wameaga rasmi soka la ushindani mbele ya mashabiki lukuki waliojitokeza kwenye mchezo maalum wa kirafiki uwanja wa Bandari-Tandika.
Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya kufungana 4-4 na kufanya mikwaju ya penati iamue mshindi.
Vikosi vyote vya timu mbili vilisheheni mastaa waliowahi kucheza ligi kuu Tanzania bara miaka mingi iliyopita na wengine ambao bado wanaendelea kucheza hadi sasa walikuwepo.
Kanali mstaafu Idd Kipingu alikuwa ni mgeni rasmi wa mchezo wa heshima wa kuwaaga Amri Kiemba na Thomas Maurice ambaye aliwahi kuwafundisha wote wawili katika shule ya Makongo na leo alikuwa akiwashuhudia wanastaafu soka. "Leo ni siku nzuri watoto wetu wanatamka rasmi kwamba wanaachana na soka la ushindani na hatimaye umati mkubwa umejikusanya kwa ajili hiyo, nawashukuru nawapongeza." "Nawashukuru wote waliojitokeza kuwapa heshima vijana wetu, kila anaeingia kwa hodi lazima atoke kwa kwaheri."
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.