Posti Ya Haji Mnara Baata Ya Taarifa Za Msiba Wa Mtoto Wa Canavaro..
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haaji Manara ameungana na maelfu ya wapenda soka nchini kumpa pole nahodha wa klabu ya Yanga kutokana na msiba alioupata wa kuondokewa na mwanae Anwar Nadir Ally aliefariki mapema leo asubuhi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu ya matatizo ya damu.
Manara ametumia ukurasa wake wa Instagram kutoa salaam zake ikiwa ni pamoja na pole kwa rejendari huyo wa soka kunako mitaa ya Jangwani..
Pole sana Nahodha wa Yanga Nadir Haroub Canavaro kwa kufiwa na Mtoto wako mwenye umri wa miezi miwili Anwar,Mm binafsi,viongozi, wachezaji,benchi la ufundi,Wanachama na mashabiki wa Simba tunaungana na ww ktk kipindi hiki kigumu kwako na kwa familia nzima,Poleni pia wanayanga wote... #NadirHarub @Yangasc @dismasten@clementsanga 🙏🙏
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.