Picha+ video: Yanga Walivyoifuata St. Louis Asubuhi Ya Leo..


KIKOSI cha Yanga sc kimeondoka asubuhi hii kuelekea Shelisheli tayari kwa mchezo wa marejeano ya ligi ya mabingwa afrika dhidi ya wenyeji St Louis.

Kwenye uwanja wa Ndege wa JKNIA Mwenyekiti wa kamati ya mashindano Hussein Nyika amesema kikosi kinaondoka kueleka shelisheli kikiwa na morari ya juu hasa baada ya matayarisho mazuri na ushindi mnono kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji.


Vijana wako fiti na wana morari ya hali ya juu, tumefanya mazoezi ya kutosha kwa muda wa siku tatu, hapo kabla tulikuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji mchezo ambao mwalimu aliutumia kurekebisha makosa aliyoyaona kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya St Louis na sasa kikosi chache kiko kamili kwenda kumaliza kazi huko shelisheli.


Kikosi cha Yanga kikiwa ndani ya ndege safarini kuelekea Shaelisheli.


No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.