Viongozi Toto African Ya Mwanza Wagawana Magodoro..


Baada ya Toto Africans ya Mwanza kushuka daraja kutoka ligi daraja la kwanza hadi ligi daraja la pili, baadhi ya viongozi wa klabu hiyo wameanza kuchukua vifaa ikiwemo magodoro.
Mwenyekiti wa mashindano Wambura Mtani amesema kuna viongozi waliosafiri na timu kwenda Dodoma na Dar wakiwa na baadhi ya vifaa, hawajavirejesha vitu hivyo baada ya timu kurejea Mwanza.
“Wapo baadhi ya watu wameanza kugawana mali za Toto, wamechukua magodoro, sasa ukianza kuchukua vitu wachezaji wanaobaki na watakaokuja kwa ajili ya ligi daraja la pili watatumia nini?”-Wambura Mtani, Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano Toto Africa.
“Tena sio wanachama tu bali ni viongozi wenye dhamana ambao wanatakiwa kuwa na uchungu na Toto, kuichangia lakini wao ndio wanakuwa wa kwanza kuchukua vitu vya klabu.”
“Wapo viongozi ambao waliondoka na timu kwenda Dodoma na baadae Dar kucheza FA Cup, kuna baadhi ya vifaa walichukua kwa ajili ya kwenda navyo nasikia havijarudi kambini.
“Tumekubaliana ikifika Jumatano mchana vofaa havijarudi, tunakwenda polisi kwa sababu huu ni wizi kama wizi mwingine.”
“Toto ni taasisi inapaswa itoke hapo ilipo ipande hadi daraja la kwanza na baadae ligi kuu kama ilivyokuwa.”

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.