Ombi la Jerry Muro kwa mashabiki na wachezaji wa Yanga
Aliyewahi kua Afisa Habari wa klabu ya Yanga ,Jerry Muro ametoa rai kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kufanya maombi na dua ili timu hiyo ili kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda katika Ligi Kuu Bara Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Muro pia ametoa ombi kwa wachezaji wa Yanga waweke fadhila mbele kuliko maslahi, wakumbuke kipi Yanga imewafanyia, na si kuendekeza pesa kwani watakuwa wanaiharibia timu malengo huku akijaribu kukumbushia Simba walikuwa wakifanya kipindi kile hali ya uchumi kwao haikuwa nzuri kama ambavyo Yanga walivyo sasa.
"Wachezaji wanatakiwa watambua hali ya kifedha ilivyo klabuni, wanapaswa wajitume zaidi Uwanjani na si kuendekeza masilahi, vema wakakumbuka Yanga imewafanyia mangapi mazuri kuliko kujikita zaidi kwenye fedha" amesema Muro.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.