Okwi Aibukia Shinyanga, Simba Ikibanwa Mbavu
Emmanuel Okwi amefunga goli lake la kwanza msimu huu nje ya Jiji la Dar es salaam katika sare ya goli 2-2 dhidi ya Mwadu Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Kambarage uliopo mkoani Shinyanga.
Katika mchezo huo John Bocco ndiye alieanza kuvunja ngome ya Mwadui fc mnamo dakika 9 baada ya kumalizia krosi sasi kutkka kwa Shiza Kichuya.
Goli hilo la Bocco lilidumu mpaka kutamatika kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza. Dakika ya 59 Mwadui walisawazisha goli kupitia kwa mpira wa adhabu uliopachikwa kambani na David Luhende.
Goli la Okwi lilipachikwa kimiani mnamo dakika ya 71 kwa mkwaju wa penati ambao uliamuliwa na mwamuzi Shomari Lawi kutokana na kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.
Lakini kutokana na bahati mbaya ya Simba katika mchezo huo ,Mwadui FC walipambana na kufanikiwa kusawazisha goli hilo kupitia kwa straika wake Paul Nonga.
Simba bado iko kileleni mwa ligi kuu Tanzania baraikiwa na pointi 42 ikiwa ni pointi 5 mbele ya Yanga wanaoshika nafasi ya pili.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.