MKUBWA HAKOSEI...!!


Ndivyo unavyoweza kusema kwa sisi waafrika hasa pale inapoonekana kabisa kua mkubwa kakosea.
Namtizama Shomari Kapombe akicheza kwa kiwango kikubwa tangu mechi ya kwanza nilipomuona akirejea toka kwenye majeraha...!
Kichwani mwangu unanijia mwangwi wa sauti ya baba yake na Shomari pale Msimbazi nna maana mwenyekiti wa kamati ya usajili wa timu pale alipokua akizungumza mambo ambayo kwangu mimi sio sawa lakini narejea kiafrika "MKUBWA HAKOSEI" Nanukuu baadhi ya maneno hayo "“Vipimo havidanganyi, yeye kama anaona hawezi kucheza basi akae pembeni, siyo anakaa anakula mshahara wa bure.
“Kama amepona acheze, kama hataki basi aondoke, majeruhi gani ambaye haponi muda wote huo!”
Alipoulizwa kuhusu vipimo vinavyosema, alisema: “Vipimo vinaonyesha ameshapona vizuri, yeye ana uwoga wake tu, labda anaogopa ataumia, msimamo wetu ni yeye mwenyewe aamue acheze au aondoke.”

Ni maneno mazito yasiyo na ladha nzuri kutoka kwa kiongozi,mzazi na baba wa kijana kuyapeleka kwa mchezaji wakati muhusika bado yupo kwenye maumivu.
Ni maneno yanayoweza kumvuruga kisaikolojia mchezaji na kumtoa kabisa katika mstari na kujikuta akipotea na kupoteza kipaji ambacho ni muhimu kwa manufaa ya timu husika na taifa kwa ujumla.
Pongezi zangu kwa Shomari ni kua amekua mwenye nidhamu na kuishi kwenye hiyo kauli mbiu kua "MKUBWA HAKOSEI".Kwa kitendo cha kupona majeraha yake na kurejea uwanjani kwa kiwango cha juu kabisa kushinda ata wale waliokua fit 100% kwa kipindi chote ni dhahiri kua amemjibu mzee wake kiutu uzima.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.