Kinyago Cha Simba Chawaandama Mbao Fc
Timu hiyo ya Mbao FC imetolewa kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) katika hatua ya 16 Bora tu baada ya kufungwa kwa penalti 6-5 kufuatia sare ya 1-1 na wenyeji, Njombe Mji FC ndani ya dakika 90 Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.
Sasa timu zote zilizocheza fainali ya ASFC Mei 27, mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma zinaipa mgongo michuano hiyo hata kabla ya hatua ya Robo Fainali.
Hiyo ni baada ya Simba, waliotwaa taji hilo kwa ushindi wa 2-1 kutolewa pia Desemba 22 kwa penalti 4-3, baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 na timu ya Daraja la Pili, Green Warriors ya Mwenge, Dar es Salaam inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) katika hatua ya 64 Bora.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.