Hii Ndio Klabu Itakayokutana Na Yanga Klabu Bingwa Afrika(CAF CL).
Mara baada ya klabu ya Yanga kufanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika sasa mabingwa hao wa Tanzania bara watakutana uso kwa uso na Klabu ya Township Rollers kutoka Botswana.
Yanga ambayo imefanikiwa kusonga mbele kwa kuwaondosha St. Louis itakutana na vibopa hao ambao wamefanikiwa kuwang'oa Al-merrikh ambao ni mabingwa wa soka Misri kwa msimu uliopita kwa jumla ya magoli 4-2 ambapo katika mchezo wa awali klabu hiyo iliibuka na ushindi wa goli 3-0, licha ya kupoteza ugenini leo kwa goli 2-1 lakini bado wamefuzu.
Kwa matokeo haya, Township Rollers watacheza na Young Africans katika raundi ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL).
Mchezo wa kwanza utachezwa Machi 6, 2018 Dar es salaam na marudiano kuwa Machi 16-18, 2018 jijini Gaborone.
Na katika kuhakikisha kuwa mpendwa msomaji wetu "Sokakiganjani" unakuwa na taarifa kamili nikuwa klabu hiyo kwa sasa inaongoza ligi kwa pointi 43 huku ikiwa imecheza michezo 18 pekee....
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.