Simba Kulipa Kisasi Cha Yanga Leo
Katika kuelekea mchezo wa leo wa nusu fainali ya SportPesa Super Cup kati ya Simba na KK Homeboys kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma amesema wapo tayari kukabiliana na klabu hiyo huku akiahidi kuongeza kiwango cha uchezaji zaidi ya kile kilichoonyeshwa na timu yake katika mchezo wa awali.
"Tulicheza vibaya, kila mmoja wetu ameliona hilo. Hatuwezi kurejea tena kwa akili hiyo. Wachezaji wote wameona tunahitaji kubadilika kwenye mechi ya mwisho," alisema Djuma.
Kwa upande wake nahodha wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema watahakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wa kesho ndani ya dakika 90.
"Penalti siyo nzuri, ni kama bahati nasibu. Tulikuwa na mpango wa kushinda ndani ya dakika tukashindwa dhidi ya Sharks lakini tutarejea tukiwa tofauti ili tuweze kushinda," amesema Zimbwe Jr
KK HomeBoyz ndiyo iliyoiondosha Yanga kwenye michuano hiyo kwa kuilaza mabao 3-1 kwenye mchezo wa ufunguzi, Juni 03 2018.
Simba na Kaka HomeBoyz zitacheza kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali utakaopigwa kwenye dimba la Afraha leo Alhamisi, Juni 07 saa saba mchana kisha kufuatiwa na mchezo mwingine wa nusu fainali kati ya Gor Mahia dhidi ya Singida United.

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.